Shalom! Yu mkini wewe Ni mmoja wa wale wanaomwamini na kumpenda sana Yesu, Kama ndivyo umefanya uamuzi wa busara Sana na Kama bado basi Wakati uliokubalika Ni sasa, saa ya wokovu ni Sasa!
Mambo ya kwanza, tuyaweke kwanza, Ni muhimu Sana kufahamu kwamba hapo mwanzo “Yesu Kristo” haukuwa anaitwa hivyo, hilo ni jina la Kazi au dhumuni ambalo Yeye alikuja kulifanya. Imeandikwa hivi; “Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21). Hapa tunaona maneno ya malaika akizungumza na Yusufu katika kumtia moyo kwamba asimwache mkewe na Kutokana na maneno hayo tunaona kwanini huyo atayezaliwa ataitwa Yesu.
Leo nataka tuone kidogo sababu kadhaa ambazo zilimfanya Yesu Kristo aje duniani katika Mwili. Mpaka hapo tu kauli hiyo iko sawa katika hali ya kutokuwa sawa, kwanini ? tulitakiwa kusema hivi “…Mungu kuja duniani katika Mwili” fuatana nami katika Somo hili:
Lakini kwanini Sasa alitakiwa kuja duniani katika Mwili ? Na hizi ni baadhi tu ya sababu za yeye kuja katika mwili:
Kwanza, Yesu Kristo alikuja kufanya kazi ya malipizi ya dhambi za wanadamu Msalabani.
Biblia inasema, “…wote wamefanya dhambi…” (Rum 3;23) yaani wanadamu wote, kwa sababu ya kosa la Adamu mmoja wote waliozaliwa naye walihesabiwa kuwa na dhambi, na kwa sababu hiyo, ilikuwa hakuna hata mmoja anayeweza kusimama na kufanya upatanisho wa dhambi za wanadamu wenzake na Mungu, kwanini ? Kwasababu hata yeye huyo ambaye angeweza kusimama bado alikuwa na dhambi Kama wengine, lakini habari njema Ni kwamba Yesu Kristo, asiye na Baba wa Kidunia(Biological Earthly Father) alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na huyo alikuwa hana dhambi tangu kuzaliwa kwake mpaka maisha yake yote na hivyo akawa ndiye pekee mwenye sifa za kuupatanisha ulimwengu na Mungu imeandikwa hivi “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” _(2Koritho 5;21)
Pili, Yesu Kristo alikuja kutupa uzima(life), hii Ni kwa kila mwanadamu ataye mwamini yeye.
imeandikwa hivi; “….. Mimi nalikuja ili wawe na uzima,Kisha wawe nao tele” (Yohana 10;10). Andiko jingine linasema hivi “Yesu akamwambia mimi ndiye njia na kweli na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya Mimi” (Yohana 14;6). Jambo hili Ni moja ya mambo Makubwa Sana ya kiroho ambayo Yesu Kristo alikuja kuyafanya, hapo mwanzo kwa sababu ya dhambi na makosa tulikuwa wafu, tumetengwa mbali na Mungu, lakini Yeye Mungu kwa kuwa Ni mwingi wa Rehema alitufufua pamoja naye akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa Roho, katika Kristo Yesu. (Efeso 2;1,5&6)
Tatu, Yesu Kristo alikuja katika Mwili ili aweze kuwa na sifa za kuwa kuhani wetu Mkuu. Hapa Kuna Jambo jingine la msingi Sana, unapotazama ujio wa Yesu Kristo hapa duniani, biblia inasema zamani tulikuwa na kuhani aliyekuwa anatoa sadaka za dhambi Kila Mwaka, lakini alipokuja Yesu, yeye aliitoa sadaka mara moja tu kwa ajili ya watu wote na sadaka hiyo hudumu hata milele, imeandikwa hivi; “Katika mapenzi hayo mmepata utakaso kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Na Kila kuhani husimama Kila siku akifanya ibada na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi, lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu.” (Waebrania 10;10-12) unaweza pia kuongeza kusoma Waebrania 4;14-15.
Nne, Yesu Kristo alikuja ili kuharibu kazi za shetani.
Biblia inasema hivi; “Basi kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye alikuwa na nguvu za mauti yaani ibilisi. Awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa” (Waebrania 2;14-15)
Na tano, Yesu Kristo alikuwa kuja kielelezo na mfano kwetu kwa habari ya Utakatifu, utumishi, maarifa, kumcha Mungu, Ushindi katika hali mbalimbali na sababu nyingine nyingi. Biblia imerekodi Kuna Maeneo alikuwa anasema “….jifunzeni kwangu…” Na hapa nakupa andiko angalau hili moja “Kwakuwa nimewapa kielelezo; ili Kama Mimi nilivyo watendea, ninyi mtende hivyo” Yohana 13;15.
Kwa leo tuishie hapo,tupatetafakari halafu, tutaendelea wakati ujao, Ubarikiwe Sana!
Written and Prepared by Robin Mwenda!


