Roho Mtakatifu ni Nani Haswa?

Bible Learning

Kuna utata mwingi kuhusu kumtambua Roho Mtakatifu. Wengine humchukulia kama nguvu fulani zisizoonekana. Wengine huamini kwamba ni uwezo wa Mungu ambao Mungu huuachilia maishani mwa wale ambao wamemwamini Kristo. Je, Biblia inasemaje kuhusu Roho Mtakatifu? Kwa kifupi, Biblia inasema kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu. Pia, Biblia inasema kwamba Roho Mtakatifu ni nafsi, yenye akili, hisia, na mapenzi yake.

Swali la kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu limo ndani ya mistari mingi ya Biblia kama vile Matendo 5:3-4. Katika mistari hii, Petro anapambana na Anania aliyemdanganya Roho Mtakatifu na anasisitiza kuwa “hukumdanganya mtu bali Mungu.” Hili ni tangazo la wazi kwamba kumdanganya Roho Mtakatifu ni kumdanganya Mungu. Tunaweza pia kujua kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu kwa kuwa anatajwa na hali sawa na za Mungu. Roho Mtakatifu yuko kila mahali kama inavyoelezwa katika Zaburi 139:7-8, “Nitaenda wapi nijifiche na Roho? Ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko.” Tena, katika 1 Wakorintho 2:10 tunaona hali ya kuwa Roho Mtakatifu yupo kila mahali, “Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake Mtakatifu. Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake? Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.”

Tunaweza kujua kwa hakika kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana akili, hisia, na mapenzi yake. Roho Mtakatifu hufikiri na hujua (1 Wakorintho 2:10). Roho Mtakatifu anaweza kuugua (Waefeso 4:30). Roho Mtakatifu hutuombea (Warumi 8:26-27). Roho Mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na mapenzi yake mwenyewe (1 Wakorintho 12:7-11). Roho Mtakatifu ni Mungu, sehemu ya tatu ya utatu wa Mungu. Kama Mungu, Roho Mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu Kristo alivyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16, 26; 15:26). Hayo ndio machache yamuhusuyo Roho Mtakatifu, Mungu astahiliye kuabudiwa.

Mungu akubariki Sana kwa kujifunza leo, usiache kutuandikia katika sehemu ya maoni nini unatamani ujifunze zaidi. 

-Spiritual Class Online-

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *