Nakusalimu katika Jina la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai. Na nakukaribisha katika Msimu wetu mpya wa SPIRITUAL CLASS ONLINE na leo tunaanza na Somo muhimu Sana ninaloamini kwamba kwa kulifahamu utapata faida nyingi sana katika kufahamu ni kwa namna gani Mungu anatusaidia katika maisha yetu ya kila siku.
Katika kuanza somo letu naomba kwanza tuangalie mistari yetu miwili ya kutuongoza. Yohana 1:17 "Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo" pia tuangalie 2Wakoritho 13;14 "Neema ya Bwana Yesu Kristo na Pendo la Mungu na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote". Maandiko hayo tuliyoyasoma yanatuonyesha Nani anatoa neema kwaajili ya watu wake. Katika 2kor 13;24, biblia inaonyesha kila nafsi katika nafsi tatu zinazosababisha utatu Mtakatifu wa Mungu wetu imebeba Jambo fulani nyuma yake. Kwanza, tunaona "Bwana Yesu" huyu amebeba Neema, pili "Mungu" (Baba) huyu amebeba Pendo, nafikiri moja ya mistari maatufu sana kwenye biblia ni ule wa Yohana 3;16 ambao unaanza kwa kusema "Kwa maana Jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu…" Hivyo nyuma ya Mungu wetu kuna upendo wa ndani sana kwa ajili yetu ambao mara nyingi unamfanya ajidhihirishe kikamilifu katika kututetea. Tatu "Roho Mtakatifu" huyu tunaona nyuma yake kuna Ushirika(fellowship). Baada ya Mungu kuupenda Ulimwengu na Kumtoa Yesu Kristo kwetu, Yesu nae alikufa,akafufuka na hatimae kwenda zake Mbinguni, lakini habari njema ni kwamba anavyoondoka hakutuacha Yatima alituachia Msaidizi(Roho Mtakatifu) ambae huyo anakaa ndani Yetu na tunashirikiana nae milele. Soma Yohana 16:7 na Yohana 14;26.
Na mstari ya 17 wa kitabu cha Yohana sura 1. Unaongea juu ya; kwanza, ujio wa torati na Pili, ujio wa Neema na Kweli. Sasa imekuwa ni Kama ufahamu wa kawaida kabisa kuona kana kwamba Dunia imekuwa na vipindi vikubwa viwili yaani Torati(toka kwa Musa) na Neema(toka kwa Yesu Kristo). Lakini lazima tukumbuke kwamba kabla ya Musa kulikuwa na watu wakubwa wengi waliofanya kazi na Mungu kwa viwango vya juu Sana. Ukifuatilia vizuri kutoka Adamu utagundua kuwa Musa alikuwa ni Kama Mtu wa 25 yoka Adamu. Nikiwa na maana Adamu mpaka Nuhu(vizazi 10), Nuhu mpaka Ibrahimu(Vizazi 9) na Ibrahimu mpaka Musa(Vizazi 6). Jumla yake ni 25 ambapo ndio tunaona Mungu akimkabidhi Musa torati.
Sasa je watu kabla ya torati waliishije ? Oh! Ni jambo la ajabu sana lakini ndio kweli na Biblia inaonyesha watu hao waliishi katika neema. Mpaka hapa naomba ufahamu maana ya Neema, neno hili kwa lugha ya asili(Greek) linaitwa "Charis" ambalo tafsiri ya kiingereza ni unmerited favour, kindness or goodness, kwa lugha yetu tungesema ni upendeleo au ukarimu na wema usio zingatia mtu amefanya nini hapo kwanza. Sasa tuendelee; Nataka nikuonyeshe mifano michache tu ya watu waliopokea neema waziwazi toka kwa Mungu kabla ya Musa na bila shaka Kabla ya kuja kwa Yesu Kristo. Katika sura ya 6 ya kitabu cha Mwanzo biblia inaongea juu ya uovu mkubwa Sana uliokuwa unafanywa na watu wale lakini Kuna jambo liliyokea kwa mtu mmoja, biblia inasema hivi Mwanzo 6;7-8 "BWANA AKASEMA, nitamfutilia mbali mwanadamu nikiyemuumba usoni pa nchi;mwanadamu na mnyama na kila kitambaacho na ndege wa angani kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA". Hilo ni moja ya andiko linaloonyesha kwamba watu walipewa Neema tangu mwanzo kabisa hata kabla ya Sheria(torati) kuja. Na mtu wa pili ni Ibrahimu, biblia inatufundisha kwamba Mungu bila kuzingatia lolote la ki-Mungu Sana ambalo Ibrahimu alikuwa amelifanya lakini Kitabu cha Mwanzo 12 kuanzia mstari wa Kwanza biblia inasema Bwana akamwambia Abram, toka wewe katika nchi yako na jamaa yako na nyumba ya Baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha. Na ukiendelea utaona Mungu anamuahidi ahadi kubwa mno na ya kwamba atambarikia Sana wakati kilindi hiki Ibrahimu bado kabisa hajafanya lolote kubwa mbele za Mungu, oh! Hakika hii ni Neema, ni upendeleo(unmerited favour).
Lakini baada ya kipindi hicho ghafla tunaona Mungu anaamua kumpa Musa torati, unaweza kujiuza hii ilikuwa ya kazi gani sasa. Lakini jibu ni kwamba ilikuwa na kazi fulani muhimu sanakioindi hicho, kwanza neno torati kwa lugha ya asili(kiebrania) ni "Torah" likiwa na maana kwa kiingereza Kama _Guardian au Instructions ambalo kwa lugha yetu ni Kiongozi au maelekezo. Na sababu kubwa za torati kuja ni pamoja na hizi hapa;
Kwanza, Torati ililetwa ili kuonyesha makosa ya watu na kuelekeza waishi kwa utaratibu. Galatia 3;19 biblia inasema "Torati ni nini basi, iliingizwa kwa sababu ya makosa hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi…". ukisoma andiko Hilo katika Amplified Bible biblia inatumia neno "Expose" thier sinfulness. Hivyo torati ilikuwa na kazi ya kuweka hadhani makosa ya watu huku Yenyewe ikiwa haina uwezo wa kuyaondoa. Biblia inasema Waebrania 10;4 "Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi".
Pili, Torati ililetwa kuwa utangulizi wa uhalisia ambao ungetakiwa kuja baadae kwa njia ya Yesu Kristo (ilikiwa kivuli). Waebrania 10:1,8-12 biblia inasema "Basi torati kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, Wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zilezile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wowote kuwa kamilisha waikaribiao" ukiendelea mpaka msitari wa 12 anamuongelea Yesu sasa akisema _"Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu".
Na tatu, Torati ililetwa kuwa kiongozi, kutuleta mpaka ujio wa Yesu Kristo.Sasa Kivipi torati ilibeba assignment kubwa kiasi hicho? Na je tunatakiwa kuitumia torati mpaka sasa? Hayo na mengine mengi katika kumalizia somo hili usikose sehemu ya pili, Bwana akubariki!
Prepared and written by;
Robin Mwenda(Man of God)
+255756814182/+255713280679


