NINI HATMA YA WALE WANAOKUFA KATIKA ULIMWENGU HUU WA SASA?

Imekuwa ni jambo la kawaida kusikia kwamba mtu fulani wa karibu au mbali amefariki kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ajali, ugonjwa au uzee na nyingine nyingi zinazofanana na hizo. Pia imekuwa kawaida sana kwetu sisi wanadamu kujali sana na kutafakari wale walioachwa na aliyefariki wataishije hapa Duniani, hali hii sio ya ajabu kwani ni ukweli usiopingika kwamba maisha lazima yaendelee kwa wale ambao bado wapo hapa duniani.

Lakini leo kwa msaada wa Roho Mtakatifu nikuombe tutazame sana na kwa undani wapi huyo aliyekufa ameelekea, hii itatufanya sisi tuliobaki ambao mara nyingi tumesikika tukisema safari yetu ni moja kujua safari hiyo ni ipi na kama kweli ni moja kwa wote au la! karibu sana tujifunze pamoja.

Kwanza kabisa, ni muhimu sana tufahamu kwamba kibiblia, tafsiri ya mwanadamu ni hii; Mwanadamu ni roho ana nafsi na anakaa katika mwili. Biblia inatuonyesha katika kitabu cha mwanzo kwamba Mungu alimuumba Mtu, *Mwanzo 1;27 " Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke aliaumba." Mchakato wa uumbaji katika kitabu cha mwanzo unaonekana kwamba Mungu alianza na kuumba mwili kwa udongo, kisha akampulizia puani pumzi ya uhai(roho) na baada ya kupuliziwa tu pumzi biblia inasema mwanadamu akawa nafsi hai, oh! Halleluyah. Hivyo mstari wa 7 wa sura ya 2 ya kitabu cha mwanzo inatuonyesha maeneo yote matatu ya mwanadamu yaani; roho, nafsi na mwili. Pia mstari huohuo unatuonyesha vizuri chanzo cha kila eneo la mwanadamu, inasomeka hivi; *Mwanzo 2;7 " Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai." Ikiwa na maana Mwili unatoka mavumbini, pumzi ya uhai(roho) inatoka kwa Mungu na nafsi ilitokea baada ya roho kukutana na mwili ndio maana eneo hili la nafsi huwa lina mambo matatu pia yaani; hisia,utashi na nia au matakwa. Sasa katika hatua ya kifo biblia inasema hivi; *Mhubiri 12;7 " nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa," halleluyah! Hivyo biblia inatujulisha wazi kwamba tunapofika mwisho wa maisha yetu hapa duniani kila sehemu huwa inarejea mahali ilipotoka yaani mwili hurejea mavumbini na roho kwa Mungu.

Sasa tuingie ndani kidogo; Bibilia inaonyesha wazi kwamba Mungu aliupenda ulimwengu uliokuwa katika hali ya dhambi na upendo wake ulimfanya amtoe mwanaye wa pekee ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele tunasoma hivi, *Yohana 3;16,18 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda uliwengu hata akamtoa mwanaye wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Amwaminiye yeye haukumiwi, bali asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. Mistari hii miwili inatuinyesha makundi mawili ya watu mbao wote kwa hatua ya kwanza wataishi hapa duniani ila maamuzi yao yatawafanya wengine Mungu awape raha ya milele na wengine hukumu ya milele. Oh! Ni maombi yangu Mungu akusaidie uamue vizuri na kwa busara ili hatimaye upewe raha ya milele.

Sasa tuanze na wale walio na watakao kubali upendo wa Mungu, yaani kumkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao.

Kama tulivyoona katika kitabu cha Yohana 3 mstari wa 18 kwamba … amwaminiye haukumiwi … na pia katika *Warumi 8;1 biblia inasema Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Hivyo kama walio katika Kristo Yesu hawahukumiwi hii inaonyesha wao wanaingia katika raha ya milele, lakini wapi hasa roho zao huenda baada tu ya kufa, je huingia mbinguni moja kwa moja au huhifadhiwa kwanza mahali fulani? Au labda zinatulia bila ufahamu mpaka siku ya Yesu kurudi ndio zifufuliwe na kuingia mbinguni?

Hebu tusome *Luka 23;43 Yesu akamwambia,amini, nakuambia, leo hivi utakuwaa pamoja nami peponi. Pia *Wafilipi 1;23 Ninasongwa katikati ya mambo mawili;ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana

To be continued…

Prepared and written by;

Robin Mwenda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *