SOMO: METANOIA (TOBA)
Nakusalimu katika Jina la Bwana Yesu Kristo, natumaini wewe umzima kabisa, na kwa Sasa karibu katika somo letu jipya kabisa lenye Kichwa cha Somo; METANOIA, Neno la kiyunani ambalo maana yake ni TOBA.
Katika kuanza somo letu naomba tusome mistari hii miwili kisha tuendelee 2Petro 3:9 "Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, Kama Wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu maana hapendi mtu yeyote apotee bali wote wafikilie toba". Pia tusome Ezekiel 14:6"Kwa sababu hiyo uwaambie nyumba ya Israel, Bwana MUNGU asema hivi; Tudini ninyi, mkageuke na kuviacha vinyago vyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu yote".
Sasa tuendelee, nimechagua mistari hii miwili kwani wa kwanza unaeleza hamu ya Mungu kwa ajili ya sisi kutubu na mwingine unatoa ufafanuzi wa neno Toba. Maandiko katika 2Petro 3:9 biblia inasema hatupasi hata mara moja kuona Kama Bwana Yesu anakawia kuja au hatakuja kabisa Kama Wengine wanavyofikiri(soma kuanzia msitari wa kwanza), Mtume Petro kwa kuwa na uwezo wa kusoma Mawazo ya Mungu juu ya watu wake anasema, huko ambako wengine wanadhani ni kukawia sio Kama wanavyodhani wao, bali ni kwamba Mungu anatuvumia ili tutubu kwanini ? Kwa kuwa Yeye hapendi mtu Yeyote apotee bali wote tufikilie toba.
Mpaka hapa naomba Sasa tuone Nini maana ya Toba Jambo ambalo Mungu analitarajia kwa kila mwanadamu na hata Sasa anavumilia ili kuona Lini mtu mmoja anaenda kupata toba. Neno "Toba" limetokana na neno la kigiriki linaloitwa "Metanoia" na kwa kiingereza ni "Repentance" neno hili maana yake ni "Change of one's Mind" yaani "kugeuka kwa nia ya Mtu". Kwa lugha ya asili neno Toba sio lazima iwe ni kugeuka Kutoka dhambini, hata hivyo ni ukweli usiopingika kwamba katika Biblia Neno mara nyingi limetumika kuonyesha mgeuko toka katika njia mbaya na kumgeukia Mungu. Katika kitabu cha Ezekiel 14:6 tunaona Mungu anavyohitaji watu wake wamrudie na kumgeukia yeye na kuachana na Miungu mingine; hiyo inaweza kuwa ni tafsiri nzuri Sana ya Toba. Mara zote matokeo ya toba ya kweli imekuwa ni mabadiliko ya Matendo ya Mtu, tabia na mfumo mzima wa maisha.
Hapa naomba niweke sawa tofauti ya Toba(Repentance) na Ukiri (Confession). Katika Muktadha wa somo letu la leo maneno hayo mawili yanatofautiana kwa namna hii; Ukiri ni hali ya mtu kukubaliana na kosa alilolifanya, japo sio lazima ageuke na kuliacha kosa hilo, yeye huishia na kusema "Ni kweli nikitenda Jambo fulani" lakini. Toba hii huenda mbali zaidi, hii ni kukubali kwamba ni wewe ulielitenda jambo na pia moyo wako unakuwa unatamani kuliacha na kuanza mfumo mpya kabisa wa maisha.
Biblia inasema hivi katika Luka 3:8 "Basi toeni Matunda yapatanayo na toba…." Soma pia katika Matendo 26:20"…Katika nchi yote ya uyahudi na Mataifa kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakiyatenda Matendo yanayopatana na kutubu kwao"_. Haleluya! Unaona kupitia mistari hii miwili tunaona kwamba toba huwa inaambatana na uthibitisho wa nje kwa kile ambacho kimetokea ndani, uthibitisho huo huwa ni Matendo yanayopatana na toba aliyoifanya mtu.
Mpendwa katika Bwana, Mungu anatamani Sana kila mmoja afikilie Toba, hivi unajua Yesu alipokuja duniani, ujumbe wake wa kwanza ulikuwa ni Toba (Marko 1:14)na alipofufuka kabla hajapaa aliwaamuru wanafunzi wake waende kwa mataifa yote wakawahubiri mataifa wafikilie toba (Luka 24:46-47) na hata Mitume baada ya Yesu kuondoka duniani, biblia inasema siku ya Pentekoste baada ya kuhubiri, watu walichomwa Sana mioyo yao na baada ya kuuliza wangetakiwa kufanya Nini, Jibu la kwanza la Mitume lilikuwa ni "tubuni" (Matendo 2:28)
Inawezekana mpaka hapa Kuna mtu anajiuliza je kutubu ndio kujuta? Hapana, japo hata kutubu Kuna muda mtu anakuwa anajutia makosa na dhambi zake ambazo amezifanya mpaka siku hiyo anatubu. Lakini kutubu huenda mbali zaidi na asili yake ni ya ki-Mungu. Toba sikuzote huwa ni directional (yaani; inampeleka mtu kwa Bwana, inamuingiza kwenye furaha ya Mungu baada ya kuwa amesamehewa makosa yake). Tofauti na majuto ambayo haya yanasababisha mtu kuchanganikiwa na kuwa na hatia bila kupata Msaada wowote. Hali hii ndio ilimpata Yuda Iskarioti hadi akaishia kujinyonga. Toba huwa inatolewa na Mungu mwenyewe na ndio maana huwavuta watu warejee kwake, biblia inasema Yohana 6:44 "Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba, aliyenipeleka; nami nitamfutua siku ya mwisho". Sasa unajua Nini? Jukumu hilo amepewa Roho Mtakatifu kwa sasa ambaye yupo hapo karibu kabisa nawe Sasa hivi. Biblia inasema atakapo kuja huyo Roho Mtakatifu ataushuhudia ulimwengu kwa habari haki, dhambi na hukumu. Lakini Je Kuna uhusiano gani kati ya Toba na Wokovu, Kuna tofauti gani kati ya kuongoka na kuokoka ? Na je Kuna hatua fulani maalumu za kufuata ili mtu apate Toba toka kwa Bwana? Hayo na mengine mengi usikose METANOIA SEHEMU YA PILI. Bwana akubariki na uhifadhiwe katika Neema yake. Amina!
Prepared and Written by
Robin Mwenda